Swift

UNAMHITAJI YESU KATIKA MELI YAKO






Maandiko
Math 14:23-33
23 Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake.  24 Na kile chombo kimekwisha kufika katikati ya bahari, kinataabika sana na mawimbi; maana upepo ulikuwa wa mbisho.  25 Hata wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akienda kwa miguu juu ya bahari.  26 Wanafunzi walipomwona akienda juu ya bahari, wakafadhaika, wakisema, Ni kivuli; wakapiga yowe kwa hofu.  27 Mara Yesu alinena, akawaambia, Jipeni moyo ni mimi; msiogope.  28 Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji.  29 Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu.  30 Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe.  31 Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka?  32 Nao walipopanda chomboni, upepo ulikoma.  33 Nao waliokuwamo ndani ya chombo wakamsujudia, wakisema, Hakika wewe u Mwana wa Mungu.

Marko 4: 35-41
35 Siku ile kulipokuwa jioni, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng'ambo.  36 Wakauacha mkutano, wakamchukua vile vile alivyo katika chombo. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja naye.  37 Ikatokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji.  38 Naye mwenyewe alikuwapo katika shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia?  39 Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.  40 Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado?  41 Wakaingiwa na hofu kuu, wakaambiana, Ni nani huyu, basi, hata upepo na bahari humtii?

Luka 5:1-9
1 Ikawa makutano walipomsonga wakilisikiliza neno la Mungu, yeye alikuwa amesimama kando ya ziwa la Genesareti, 2 akaona vyombo viwili vimekaa kando ya ziwa, lakini wavuvi wametoka, wanaosha nyavu zao.  3 Akaingia katika chombo kimoja, ndicho chake Simoni, akamtaka akipeleke mbali kidogo na pwani. Akaketi, akawafundisha makutano ali chomboni.  4 Hata alipokwisha kunena, alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki.  5 Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu.  6 Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika;  7 wakawapungia mikono washirika wao waliokuwa katika chombo cha pili, waje kuwasaidia; wakaja, wakavijaza vyombo vyote viwili, hata vikataka kuzama.  8 Simoni Petro alipoona hayo, alianguka magotini pa Yesu, akisema, Ondoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mtu mwenye dhambi, Bwana.  9 Maana alishikwa na ushangao, yeye na wote waliokuwa pamoja naye, kwa sababu ya wingi wa samaki walioupata;

UNAMHITAJI YESU KWENYE MELI YAKO
Meli ni wokovu, Nahodha (dereva) ni Yesu
Bila nahodha meli haiwezi kufika, nahodha anapokuwa hayuko makini basi is shida.




KUWA KAMA MTOTO ILI UMWONE YESU
1.       Utangulizi
Kila mmoja anatamani kuingia mbinguni. Hata mchawi/jambazi anatamani hilo.
Wengi wanaamini kuna maisha baada ya kifo japo wanashindwa kutii amri za Mungu.
Kwa nini Yesu alisemaa ni watu kama watoto ? watoto wana tabia specific ambazo zinampendeza Mungu na wanadamu.
Tabia za mtoto
Hawasemi uongo – watoto wanasema kile wanachokiona. Mfano, ukimwambia mtoto akija mgeni mwabie sipo. Akija mgeni atamwambia baba yuko ndani ila amesema akija mgeni nimwambie hayupo.
Hawana hatia -  mtoto mdogo hana dhambi na hajui dhambi. Mtoto mdogo hahukumiwi na chochote.
Hawadaiwi na mtu yeyote – watoto wote husubiri
Watoto ni wepesi kupokea maagizo………………..
Watoto ni wepesi kutii
Watoto wadogo ni wepesi kusamehe. Hata ukimwadhibu, baada ya muda mfupi anakuja mnakaa pamoja
Watoto wadogo

UKISHAPATA MUUJIZA MFUATE YESU KRISTO

Mathew 16:31-34 Mkutano wakawakaripia, wanyamaze. Lakini wao wakazidi kupaza sauti, wakisema, Uturehemu, Bwana, mwana wa Daudi!  32 Yesu akasimama, akawaita, akasema, Mnataka niwafanyie nini?  33 Wakamwambia, Bwana, twataka macho yetu yafumbuliwe.
 34 Yesu akawahurumia, akawagusa macho yao; mara wakapata kuona, wakamfuata.
Mathayo 4:25 Na makutano mengi wakamfuata, kutoka Galilaya, na Dekapoli, na Yerusalemu, na Uyahudi, na ng'ambo ya Yordani

Mathayo 19:2 Makutano mengi wakamfuata, akawaponya huko.

Mathayo 20:29 Hata walipokuwa wakitoka Yeriko mkutano mkubwa wakamfuata.

Mathayo 20:34 Yesu akawahurumia, akawagusa macho yao; mara wakapata kuona, wakamfuata.

Yohana 1:37 Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu.

Yohana 6:2 Na mkutano mkuu wakamfuata, kwa sababu waliziona ishara alizowafanyia wagonjwa.

UCHAMBUZI WA KITABU CHA YOHANA

Chapter 1
Umungu wa Yesu kama neno
Mafundisho ya Yohana Mbatizaji

Chapter 2
Harusini kana na muujiza wa divai nzuri
Yesu afukuza wafanyabiashara hekaluni

Chapter 3
Nikodemu aenda kwa Yesu usiku,
Yesu ahubiri kuzaliwa mara ya pili

Chapter 4
Yesu azungumza na mwanamke msamaria na kutaka ampe maji.
Yesu ahubiri juu ya ibada katika Roho
Yesu anayo maji ya uzima
Muujiza wa pili wa Yesu wa kumponya binti wa akida


Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
1 Baada ya hayo palikuwa na sikukuu ya Wayahudi; naye Yesu akakwea kwenda Yerusalemu.
 2 Na huko Yerusalemu penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiebrania Bethzatha, nayo ina matao matano.
 3 Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, nao waliopooza, wakingoja maji yachemke.
 4 Kwa maana kuna wakati ambapo malaika hushuka, akaingia katika ile birika, akayatibua maji. Basi yeye aliyeingia wa kwanza baada ya maji kutibuliwa, akapona ugonjwa wote uliokuwa umempata.
 5 Na hapa palikuwa na mtu, ambaye amekuwa hawezi muda wa miaka thelathini na minane.
 6 Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima?
 7 Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu.
 8 Yesu akamwambia, Simama, jitwike godoro lako, uende.
 9 Mara yule mtu akawa mzima, akajitwika godoro lake, akaenda. Nayo ilikuwa ni sabato siku hiyo.
 10 Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwambia yule aliyeponywa, Leo ni sabato, wala si halali      kwako kujitwika godoro.
 11 Akawajibu, Yeye aliyenifanya kuwa mzima ndiye aliyeniambia, Jitwike godoro lako, uende.
 12 Basi wakamwuliza, Yule aliyekuambia, Jitwike, uende, ni nani?
 13 Lakini yule mtu aliyeponywa hakumjua ni nani; maana Yesu alikuwa amejitenga, kwa sababu palikuwa na watu wengi mahali pale.
 14 Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi.
 15 Yule mtu akaenda zake, akawapasha habari Wayahudi ya kwamba ni Yesu aliyemfanya kuwa mzima.
 16 Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwudhi Yesu, kwa kuwa alitenda hayo siku ya sabato.
 17 Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi.
 18 Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu. Basi Yesu akajibu, akawaambia, Amin, amin, nawaambia,
 19 Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile.
 20 Kwa kuwa Baba ampenda Mwana, naye humwonyesha yote ayatendayo mwenyewe; hata na kazi kubwa zaidi kuliko hizo atamwonyesha, ili ninyi mpate kustaajabu.
 21 Maana kama Baba awafufuavyo wafu na kuwahuisha, vivyo hivyo na Mwana awahuisha wale awatakao.
 22 Tena Baba hamhukumu mtu ye yote, bali amempa Mwana hukumu yote;
 23 ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana hamheshimu Baba aliyempeleka.
 24 Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.
 25 Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai.
 26 Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake.
 27 Naye akampa amri ya kufanya hukumu kwa sababu ni Mwana wa Adamu.
 28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.
 29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.
 30 Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka.
 31 Mimi nikijishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu si kweli.
 32 Yuko mwingine anayenishuhudia; nami najua ya kuwa ushuhuda wake anaonishuhudia ni kweli.
 33 Ninyi mlituma watu kwa Yohana, naye akaishuhudia kweli.
 34 Lakini mimi siupokei ushuhuda kwa wanadamu; walakini ninasema haya ili ninyi mpate kuokoka.
 35 Yeye alikuwa taa iwakayo na kung'aa, nanyi mlipenda kuishangilia nuru yake kwa muda.
 36 Lakini ushuhuda nilio nao mimi ni mkubwa kuliko ule wa Yohana; kwa kuwa zile kazi alizonipa Baba ili nizimalize, kazi hizo zenyewe ninazozitenda, zanishuhudia ya kwamba Baba amenituma.
 37 Naye Baba aliyenipeleka amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wo wote, wala sura yake hamkuiona.
 38 Wala neno lake hamnalo likikaa ndani yenu, kwa kuwa ninyi hammwamini yule aliyetumwa na yeye.
 39 Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia.
 40 Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima.
 41 Mimi siupokei utukufu kwa wanadamu.
 42 Walakini nimewajua ninyi ya kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu.
 43 Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo.
 44 Mwawezaje kuamini ninyi mnaopokeana utukufu ninyi kwa ninyi, na utukufu ule utokao kwa Mungu aliye wa pekee hamwutafuti?
 45 Msidhani kwamba mimi nitawashitaki kwa Baba; yuko anayewashitaki, ndiye Musa, mnayemtumaini ninyi.
 46 Kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu.
 47 Lakini msipoyaamini maandiko yake, mtayaamini wapi maneno yangu?


You Might Also Like

0 comments